Wakazi katika Kaunti ya Pokot Magharibi wanazidi kuhimizwa kuasi mila potovu ya ukeketaji na kuwaoza wanao wasichana mapema na badala yake kuwaelimisha kwa manufaa ya baadaye.Shirika la Kyle Gabriel Foundation kupitia mradi wa IMARIKA wameweza kuwaelimisha wakazi wa kijiji cha Chepukat na Chesra katika wadi ya Chepareria kuhusu madhara ya ukeketaji na umuhimu wa kupeleka mtoto wa kike shule.Kulingana na Emily Laktabai,wana programu kadhaa mojawapo ikiwa kuwainua kina mama katika makundi tofauti tofauti, kutoa hamasisho katika jamii ya wafugaji kuhusu shida ambazo mtoto wa kike anapitia wakati anapitishwa katika ukeketaji na ndoa za mapema.'Tumekuja kuelimisha jamii ya wafugaji athari za ukeketaji pamoja na ndoa za mapema kwa mtoto wa kike,'' Laktabai alisema.Shirika hilo limelenga kuleta mbinu na jinsi jamii inaweza kukataa mila hizi na kuhakikisha kwamba mtoto msichana anapata nafasi sawa na yule wa kiume shuleni akisema kuwa masomo yanaleta mabadiliko makubwa katika jamii.Aidha wamehimiza jamii kw a jumla wageukie kuwapeleka wanao shuleni ikiwa wanatamani watoto wao wapate nafasi nzuri za kazi siku za usoni.'Tungependa kuhimiza wale ambao bado wanaendesha mila hizi potovu wageukie kuwapeleka wanao shuleni na ninaamini kupitia masomo watoto hao watafaulu,'' Laktabai alisisitiza.Kwa upande wake Mercy Kiyapyap mkazi katika kaunti hio amerai wazazi na vijana wajiunge katika kufanya kampeni za Kupiga vita ukeketaji na ndoa za mapema pamoja na kuwapa watoto fursa ya kwenda shuleni.Vilevile ameomba serikali kuingilia kati katika kuwasaka wale watoto ambao wanatoka katika familia zisizojiweza ili wasikose nafasi ya kusoma kwa sababu ya umaskini.'Tunaomba pia serikali ijitokeze katika kuwatafuta watoto ambao wanatoka familia maskini ili tuhakikishe kwamba hakuna mtoto anabaki nyumbani kwa sababu ya umaskini,' alisema kiyapyap.Kwa upande wake Chifu, Laurence Menach alisema kuwa wamekuwa katika safari kila uchao katika kuelimisha jamii kuhusu athari za ukeketaji na ndoa za mapema.Wenyeji vilevile wame toa shukrani zao kwa shirika hilo wakisema wanaamini kuwa mafunzo hayo yatazaa matunda.Aidha waliomba shirika hilo kuwajengea bweni katika shule ya wasichana ya Chepukat wakiamini kuwa mikakati kama hio itasaidia pakubwa katika kuzuia ukeketaji na ndoa za mapema.Source: Kenya News Agency
Related Articles
The Ministry of Foreign Affairs and the Kastor Group sign a memorandum of understanding for the construction of the Burkina house in Dakar
Ouagadougou: Minister of Foreign Affairs Karamoko Jean Marie TraorĂ© and the General Administrator of the Kastor Africa group, signed yesterday Friday, a memorandum of understanding for the construction of a modern real estate complex, called “Maison d…
Democracy in Action: Millions of Ethiopians Turnout as Nation Votes in 7th General Election
Addis ababa: As dawn broke over Ethiopia on Monday, a quiet but powerful movement was already underway. From the bustling streets of Addis Ababa to the shores of Lake Tana in Bahir Dar, from the historic city of Harar to the expanding urban centers of…
Desert Locust situation update 3 September 2021
BANDS LIKELY IN INACCESSIBLE AREAS OF NE ETHIOPIA A few small immature swarms persisted in northern Somalia where control operations declined. Although small-scale breeding was underway in Sudan, Chad, and Yemen, no breeding was detected in other summer breeding areas in West Africa and along the Indo-Pakistan border despite good rains. The primary concern remains […]
